Kwa mujibu wa ripoti kotoka katika Idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, waislamu wa madhehebu ya Shia mjini Hyderabad, Pakistan walifanya maandamano ya kuonesha upingaji wao dhidi ya kitendo hicho kilichofanywa na utawala wa Aal-Saud, na walitoa wito wa kufanyiwa ukarabati wa haraka kwa eneo hilo tukufu.
Wazungumzaji katika marasim hiyo waliashira kwaamba, tarehe 8 Shawwal inatambulika kama moja ya siku za huzuni katika historia ya uislamu huku wakieleza kuwa: Kubomolewa kwa makaburi ya Ahlul Bayt (a.s) katika eneo la Baqi' haikuwa tu ni suala la tofauti ya kifiqhi, bali lilikuwa ni tukio la kisiasa linaloashiria uadui wa wazi dhidi ya familia ya Mtume Muhammad (s.a.w), walisisitiza kuwa kuyatunza na kuyajengea upya maeneo hayo ni jukumu la kidini, kimaadili, na kibinadamu kwa waislamu wote Duniani.
Maoni yako